Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawzat, sehemu za taarifa za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuhusu ushindi wa mwisho wa watu wa Gaza zimewasilishwa katika makala haya.
“Suala la Gaza, kwa upande mmoja, ni suala la uonevu, kwa upande mwingine, ni suala la nguvu. Adui alitaka kuwalazimisha watu hawa kujisalimisha, kuinua mikono yao, lakini hawakuinua mikono yao, hawakujisalimisha ... subira na uaminifu huu vitawafikia. Hii itawafanya washinde na hatimaye watashinda uwanjani".
"Katika suala la Gaza, katika Hadithi ya Kimbuga cha Al-Aqsa, utabiri unajionyesha polepole. Tangu awali, utabiri wa waerevu wa dunia, sawa sawa iwe hapa au penginepo, ulikuwa kwamba katika kadhia hii, atakayeshinda ni (Upinzani) Muqawamah wa Palestina, na atakayeshindwa ni Utawala haram na muovu wa Kizayuni na uliolaaniwa".
Mwenyezi Mungu atauonyesha ushindi huu kwa Umma wote wa Kiislamu katika muda si mrefu ujao na utazifurahisha nyoyo za Taifa la Palestina na watu madhulumu wa Ghaza.
"Hakika Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya Haki / Kweli"; Wale wasioamini Ahadi ya Mwenyezi Mungu wasikudhoofishe kwa upotovu wao. Na (Insha Allah), Mwenyezi Mungu akipenda ushindi wa mwisho na usio wa kuchelewa utakuwa pamoja na watu wa Palestina na Palestina".
Your Comment